MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA NA MUONEKANO MZURI NA MARIDADI.


ACHA KUVAA KAMA MTU MWINGINE.
Siri ya urembo ni kuwa wewe Jitafute, unapendeza ukivaa mavazi yapi na ambayo yatakufanya uwe huru popote! na kumbuka kila mtu ana uzuri wake.

Acha kabisa kutaka kufanana na fulani Kwanza kila mmoja akiamua kusimamia style yake ndio tunapata taste mbalimbali za fashion na kwenda next level.

ACHA KUVAA MAVAZI YASIYOSIZE YAKO 

Jitahidi upate size yako, mfano ukivaa nguo ambayo sio size yako unaweza kuonekanaka tofauti na umri wako. Hapa tofautisha zile designs kama boyfriend jeans, shirts nk.

Lakini pia ukivaa mavazi yanayokubana umbo lako halitaonekana vile lilivyozuri, ukibanwa sana unaweza onekana una hips za tumbo au zile pingili za tumboni (handles)zikaonekana kwenye maeneo ya mbavu na mgongoni.

ACHA KUVAA KACHUMBARI

Tunaposema kuvaa kachumbari mfano, sketi au suruali inamaua Maua mengi na rangi nyingi nyingi alafu pia blause au shati pia lina maua na rangi nyingi yaani kiujumla nguo ya juu na ya chini haviendani.

Labda kama wewe ni mtaalamu wa kupangilia hizo rangi na maua yake, kama huwezi pangilia chagua nguo zenye rangi chache sana ikiwezekana katika muonekano zisizidi rangi tatu.

Zingatia pia rangi ya ngozi yako inaumuhimu katika kuchagua rangi ya mavazi yako ili upate muonekano mzuri na wakuvutia.

ACHA KUVAA ACCESSORIES NYINGI NYINGI.

Chagua accessories chache na za muhimu. Mfano hereni, cheni na saa nzuri. Ukizidisha utaonekana una makoro makoro na utaharibu muonekano wako. Pia unaweza kuwa umevaa mavazi mazuri na ya gharama lakini accessories zako mbaya zisizokuwa na ulazima zikaharibu na ukaonekana cheap.

Unaweza kuwa umevaa mavazi ya bei ya kawaida lakini ukizingatia mpangilio basi muonekano wako utakuwa wa thamani Sana. Zingatia mpangilio.

0/Post a Comment/Comments