Chanzo: Binagi Media
Wafuasi
wa Mhubiri Diana Bundala maarufu Mfalume Zumaridi wamemuandalia sherehe
ya kumshukuru Mungu baada ya kutoka gerezani ambapo alikaa kwa muda wa
mwaka mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jumanne Juni 27, 2023 Mfalme Zumaridi alisema
wafuasi wake wameandaa sherehe hiyo kumshukuru Mungu kwa kumsaidia
kutoka gerezani.
Alisema
sherehe hiyo itafanyika Julai 08, 2023 nyumbani kwake Mtaa wa Bugugu
uliopo katika Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana ambapo itahudhuriwa na
zaidi ya watu 2,000.
"Nimekaa
kwa muda mrefu bila kuongea na waandishi wa habari, nimewaita ili
kuzungumza nanyi kuelekea kwenye sherehe hii kubwa ya Shukurani kwa
Mungu wangu aliyenisimamia na kunivusha kwenye magumu mengi niliyopitia"
alisema Zumaridi.
Alisema sherehe hiyo ya kihistoria itaambatana na keki iliyobeba ujumbe wa maisha yake.
Pia
Mfalume Zumaridi alitumia fursa hiyo kuwaombea waandishi wa habari ili
wazidi kufanya kazi kwa weledi na kuwaelusha na changamoto pamoja
kuombea amani na utulivu wa Taifa ambayo ni tunu iliyowekwa na Mwenyezi
Mungu.
Na Hellen Mteleko, Mwanza
Chapisha Maoni